Kiongozi huyo wa zamani aliiongoza nchi yake kujipatia Uhuru lakini
baadaye akashutumiwa kwa kukiuka haki za kibinaadamu na kuharibu uchumi
wa taifa lililokuwa likinawiri.
Alifariki akiwa na umri wa miaka
95 nchini Singapore mapema mwezi Septemba. Jeneza lake lililokuwa na
rangi ya shaba lilishushwa kaburini.
Robert Mugabe alikuwa amezungukwa na mkewe Grace, watoto na watu wa
karibu wa familia yake. Ni marafikize wachache wa zamani waliohudhuria
mazishi hayo.
Alizikwa katika eneo la nyumba ya familia yake. Ni
wachache ambao wangedhania mtu mwenye haiba kama yake angezikwa na watu
wachache.
Baadhi wanasema kwamba ilikuwa taarifa yake ya mwisho
ya kisiasa. Kitu ambacho kitakumbukwa katika historia ni kwamba Mugabe
alikuwa mchezaji wa chess ambaye hakukubali kushindwa
Wakati alipopinduliwa mwezi Novemba aliondoka bila kutaka. Amezikwa mbali na marafikize ambao anaamini walimsaliti.
Baada ya kifo chake familia yake ililamika hadharani kuwa haikushauriwa kuhusu mipango ya mazishi yake ya kitaifa.
Katika
taarifa familia hiyo iliilaumu serikali kwa kutumia nguvu kupanga
mazishi ya Mugabe katika makaburi ya mashujaa kinyume na "matakwa yake
[Mugabe]".
Taarifa hiyo aidha ilisema kuwa ombi lake la mwisho
lilikua la mke wake , Grace Mugabe, kutoondoka kando ya jeneza lake hadi
atakapozikwa.
Robert Mugabe alikuwa rais wa kwanza wa Zimbabwe
Mwaka 1980, Bw Mugabe alishinda uchaguzi na kuwa waziri mkuu.
Mwaka 1982 aliushutumu upinzani kwa kujaribu kupindua serikali.
Maelfu ya watu waliuawa alipolituma jeshi lake lililopata mafunzo Korea Kaskizini, kuwakandamiza maadui zake.
Mwaka 1987,alibadilisha katiba ili imruhusu kuwa rais na kuongeza mamlaka yake.
Uchumi ulidororeka baada ya mwaka 2000…
Wakati Mugabe aliagiza kunyakua mashamba yaliomilikiwa na watu weupe yaliyokuwa kinara katika uchumi.
Mfumuko wa bei ulipelekea sarufi ya taifa kuwa bila thamani na hali nchini humo ikazidi kudororeka.
Baada ya uchaguzi wa mwaka 2008, Mugabe alilazimika kugawanya mamlaka na kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai.
Japo kulikuwa na ghasia dhidi ya wafuasi wa Bw Tsvangirai katika kampeni za uchaguzi.
Ndoa
yake na Grace Mugabe ,anayemzidi kwa maika 40, yaweza kuwa iliyomponza,
Wengi walikasirishwa na Grace kuandaliwa kuwa mrithi wake.
Mugabe aliapa kuwa Mungu peke yake ndio angeweza kumtoa madarakani.
0 Comments